Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
AG FELESHI ATAKA WANANCHI WASIZUNGUSHWE
service image

Na  Mwandishi  wetu

Nyerere Square

22/1/2022

Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe, Jaji Dkt.  Eliezer Feleshi  amewataka Mawakili wa Serikali  wanaotoa   huduma  katika wiki la utoaji  elimu na  maonyesho  ya Sheria ambayo yameanza leo ( Jumapili)    katika Viwanja vya Nyerere  Jijini Dodoma,  kutowazungusha wananchi wanaokwenda kupata ushauri  na  msaada wa Kisheria.

Ametoa maelekezo hayo  wakati alipokuwa akizungumza na  Mawakili wa Serikali  wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanaotoa huduma katika Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika Viwanja hivyo vya Nyerere.

“Nisingependa kuona au kusikia  mwananchi  anazungushwa,  akija mteja hapa  na shida yake   lakini  mkagundua  kwamba shida yake inapaswa kushughulikiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka au Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali  basi mmoja wenu ainuke akamchukue Wakili wa Ofisi husika aje hapa badala ya  kumzungusha mteja”

Amebainisha  kwa kusema  hatua hiyo  inapashwa  pia kuchukuliwa na  Ofisi ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili  Mkuu  kwa kubadilishana  wateja  na  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali badala ya kuwazungusha  ningependa ushirikiano huu muwe nao  katika Taasisi zote.

Vile vile  Mwanasheria  Mkuu wa Serikali  amesema asingependa kupata aibu ya kukosekana  kwa wakili  wa Serikali  katika Banda la  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Sitaki aibu,  wakati wote muwepo katika banda ili mtoe huduma kwa wananchi watakaokuja,  haitapendeza  mwananchi hanafika hapa  na  hakuna  mtu” amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali  ametembelea  banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  na Mabanda  ya Taasisi nyingine.

Kabla ya kutembelea  Mabada  nayo  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  alikuwa mmoja wa Viongozi walioshirikia maandamano yaliyoanzia katika Jengo  la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma na kumalizikia katika Viwanja  vya Nyerere.

Maadhimisho ya Siku ya Sheria yamezinduliwa  leo na Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Isidori Mpango na Kilele Chake ni  Februri Mosi,2022 katika  Uwanja wa Chinan’gali jijini  Dodoma na  Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa  Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli mbiu ya Maadhimisho  hayo ni “ umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi katika kukuza Uchumi Endelevu Wajibu wa Mahakama na Wadau.

Banda la  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali linahudumiwa na  Mawakili wa Serikali kutoka Divisheni ya  Mikataba, Divisheni ya  Uratibu na Ushauri wa Kisheria na Divisheni ya Uandishi wa Sheria na   maafisa wa kada nyingine.

mwisho

 

22 Jan, 2023
Maoni