Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
HUDUMA ZA KISHERIA KUWAFIKIA WANANCHI WALIPO-WAZIRI NDUMBARO
service image

Na Mwandishi Maalum

Wizara ya Katiba na Sheria imeahidi  kuendelea kushirikiana na Taasisi zake katika kuhakikisha huduma za kisheria  zinawafikia wananchi  kwa wakati na mahali walipo.

Ahadi hiyo imetolewa hivi karibuni  na  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndubaro (Mb) wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi  la Jengo  la Kituo Jumuishi  la Taasisi za Kisheria za  Serikali  linalojengwa Mkoani Mwanza.

Waziri Ndumbaro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo amebainisha kuwa,   Dira na Dhima za Wizara hiyo zinalenga kufanya  upatikanaji wa haki  nchini unakuwa   mwepesi na wa haraka

Akinukuu  Dira na Dhima ya Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Ndumbaro  alisema.“ Dira inasema “ Katiba na Sheria Wezeshi kwa Maendeleo ya Taifa” na Dhima inayosema “Kuwa na Mfumo Madhubuti wa Kikatiba na Kisheria wenye kufanikisha mpango wa Maendeleo ya Taifa. Ni Dhahiri kuwa Dira na Dhima za Wizara zinalenga kufanya lengo la upatikanaji wa haki katika nchini yetu kuwa mwepesi na wa haraka”Akaeleza Waziri

Ni kwa sababu hiyo,  akasema , Wizara imeendelea kuimarisha miuondombinu katika kuhakikisha upatikanaji wa haki unakua mwepesi na haraka kwa kila mwananchi.

 “Kutokana na hili, nipende kutoa Shukrani kwa Serikali wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imeendelea kutoa fedha kwa Mahakama Pamoja na  Taasisi  nyingine za  kisheria ambapo miradi mbalimbali imeendelea kujengwa ikiwemo ujenzi wa Vituo Jumuishi katika Mikoa mbali mbali”.

Pamoja na  kuishukuru  Serikali Kuu kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa vituo  Jumuishi vya Taasisi za Kisheria za Serikali.  Waziri Ndumbaro  pia  amempongeza na kumshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kufanikisha  kuanza kwa ujenzi wa vituo jumuisha

“Nitumie fursa hii kukupongeza Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa jitihada na hatua ulizozichukua za kuhamasisha uwepo wa vituo jumuishi kwa lengo la kutoa huduma za kisheria katika eneo moja (one stop Centre). Si kila mtu anawezaa kuwa na wazo na  kulitekeleza Hongera sana!.

Awali akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria kuweka jiwe la  Msingi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Mhe. Jaji Dkt. Elizer Feleshi alieleza kuwa, hatua hiyo ya kuwa na Vituo Jumuishi kwaajili ya Taasisi  za  Serikali  zinazotoa huduma za kisheria itapunguza gharama za uendeshaji.

“Kwa taasisi zote za kisheria kuwa katika Jengo  moja,  pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji,   pia kutapunguza gharama kwa wadau wetu  kwani wataweza kupata huduma katika jengo moja tofauti na ilivyo sasa”. Akasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akaongeza kuwa   kwa kutambua changamoto inayozikabili Taasisi za kisheria ikiwamo ya kutokuwa na  miundombinu ya Ofisi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia wazo la kuwa na Mpango wa kujengwa kwa majengo yatakayokuwa Vituo Jumuishi vitakavyotumiwa na Taasisi za  Kiserikali  zinazotoa huduma za Kisheria.

“Hivyo uwekaji wa Jiwe la  Msingi katika Kituo Jumuishi Mkoani Mwanza,  ni  utekelezaji wa maagizo ya  Mhe Rais Pamoja na  maazimio ya Timu ya Serikali ya Sheria ambacho ndicho chombo pekee cha Kisheria kinachojadili  masuala ya kimkakati  na kufanya maazimio ya kuziwezesha Taasisi husika kutekeleza  kwa ufanisi  majukumu yake” akasisitiza  Mwanasheria Mkuu.

Akizungumzia  matumizi ya Rasilimali zilizotumika katika ujenzi wa kituo hichyo, Mwanasheria Mkuu amebainisha kuwa matumizi yamehusisha fedha kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (fungu16) na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka fungu 35).

“ Ujenzi wa  Majengo ya  Vituo Jumuishi yanayojengwa katika mwaka huu wa fedha  kupitia fungu 16 yakihusisha jengo  hili la Ilemela Mwanza pamoja na  Arusha ambapo kiwanja hiki cha Ilemela kinamilikiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ( Fungu 35) huku fedha za ujenzi  kwa ridhaa ya Mlipaji  Mkuu wa Serikali zikitoka Fungu 16 yaani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali”.

Jengo hilo ambalo  ni la ghorofa tatu litakapokamilika litatumiwa na  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikalia na Ofisi ya Kabadhi Wasii Mkuu ( RITA)

Hafla ya uwekaji  wa jiwe la Msingi  ilihudhuriwa  pia na Mhe. Dkt. Ntemi Nihimilwa  Kilekamajenga,  Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza,  Dkt. Evaristo Longopa, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Sylvesta Mwakitalu  Mkurugenzi  Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,  Dkt. Boniface Luhende Wakili Mkuu wa Serikali  na Kabidhi Wasii Mkuu na Mtendaji Mkuu  Bi. Anjela Anatory.

01 Dec, 2022
Maoni