Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali
MSAJILI MKUU WA MAHAKAMA ATEMBELEA BANDA LA OMMS
service image

Na Mwandishi wetu

Nyerere Square

24/1/2023

 

Katika siku  ya Tatu  ya maonesho  ya  Wiki la  Sheria, Banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  limetembelewa na  Msajili Mkuu wa  Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Chuma

Wakili wa Serikali Angela Kimarao  ndiye aliyetoa   maelezo  kuhusu  majukumu ya jumla ya  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  lakini pia akabainisha  jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali zikiwamo za  kusimamia usuluhishi wa migogoro  baina ya  taasisi za  serikali.

Wakili wa Serikali  Angela   Kimaro pia alimueleza Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania   kwamba,  katika eneo la utoaji huduma za msaada wa kisheria  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  pia inayo namba ya bure   ambayo wananchi wanaweza kupiga simu  na kuomba ushauri au msaada wa kisheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pia alielezea    majukumu mbalimbali ambayo OMMS inaendelea kutekeleza   kuwa ni pamoja na  kutafsri sheria kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya   Kiswahili  pamoja , Urekebu wa Sheria mbalimbali na upembuki wa mikataba.

Kwa  Upande  wake Mhe Wilibert  Chuma alitaka kupata ufafanuzi  wa namna  gani  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  inachukua jukumu  la kuwaelimisha wananchi   utofauti kati  ya   Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na  Ofisi ya Wakili  Mkuu wa Serikali .

Vilevile Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania alitaka  kufahamu kama kumekuwa na  upungufu wa   mashauri yanayoihusu serikali  kufuatia Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoka Mwongozo wa mwaka 2020 ambao ulitoa maelekezo kwa Taasisi za serikali  kuchukua njia mbadala  za  usuluhishi badala ya kukimbilia mahakanami.

Msajili wa  Mahakama aliridhishwa na   ufafanuzi aliopewa na akaipongeza  Ofisi  ya Mwanasheria Mkuu kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake. ikielimisha umma  kuhusuAkiwa katika Banda la OMMS alielezwa kwa  muhtasari  kuhusu majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika ujumla wake.

Pamoja na  ugeni wa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Banda la OMMS limepokea   wananchi wa kada mbalimbali  waliofika  kuomba ushauri na msaada wa kisheria au   walitaka kuelimishwa  majukumu ya  Mwanasheria  Mkuu wa Serikali. Vile vile Mhasibu wa Muda wa Chama cha Mawakili wa Serikali  Irene Lesulie ameshirikia na  Mawakili wa Serikali  kutoka  OMMS katika kuwahudumia wananchi  

Imeandaliwa na  Kitengocha Mawasiliano

24 Jan, 2023
Maoni